#SemaNaRaey: Nilikatakata Elfu Ishirini Na Tano Baada Ya Kukosana Na Bwanangu

Mwanamke mmoja alimshangaza mtangazaji Annita Raey alipofichua alichofanya ili kulipiza kisasi kwa mumewe baada ya wawili hao kukosana.

Hayo yalitokea wiki iliyopita katika kipindi cha Sema na Raey huku mada kuu ikiwa waskilizaji wazungumzie vitendo ambavyo wamewahi fanya baada ya kukosana na wapenzi wao.

Mwanadada mmoja alifichua kuwa kinyume na chenye wengi hufanya ikiwemo kutafuta mpango wa kando, yeye hasira zake zilimuonesha kukata kata fedha za mumewe. Isitoshe, alivunja vunja saa ya ukuta.

"Nilijiuliza nifanye nini kwa hii nyumba? Nilichukua saa ya ukuta yenye anapenda kutoka kazini kuiangalia nikaivunja nikaiweka hapo chini. Nikasema ni nini nifanye cchenye kitamkasirisha sana, nikachuku pesa alikuwa amenipa shilingi elfu hamsini.

Nikachukua elfu ishirini na tano nikakata kata nikawekelea kwa meza. Nikachukua elfu ishsirini na tano zenye sikuwa nimekata nikaweka pamoja na hizo zingine na aliporudi kutoka kazini, nilidhani atanipiga lakini tangia siku hiyo hajawahi nikosea kwa mda wa miaka miwili.' Alijieleza mwanadada.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be