#SemaNaRaey: Nilimkatia Pastor Wangu Na Akaingia Box

Katika kipindi cha Sema Na Raey siku ya Jumatatu, mjadala mkuu ulikuwa kuhusu wanawake ambao wameolewa na bado wana mipango ya kando.

Huku mada ikiwa imeshika moto, mwanamke mmoja alifichua kuwa yeye ana mpango wa kando na isitoshe mwanaume yule ni mchungaji.

"Wanawake tumeolewa lakini bado tuna mipango za kando. Nina umri wa miaka 34 na nimekuwa kwa ndoa ya miaka minane." Alisimulia.

Tena mwanaume yule ni pastor ambaye tulianza uhusiano mwaka uliopita mwezi wa nane." Aliongeza huku akisisitiza kuwa haoni ubaya wowote wa uhusiano ule, kwani mhubiri ndiye anayemchezea mwenyezi mungu.

Isitoshe mwanamke mmoja kwa jina Mary alifichua kuwa wanawake ndio wanaowatongoza wahubiri, kwa mtindo wa nguo zao na tabia kadha wa kadha.

"Nilikuwa nashiriki katika kanisa moja ambalo sitataja, sasa nilikuwa namtongoza pastor na akaingia box." Alisema Mary. Nilikuwa namvutia na mavazi na jinsi nilivyokuwa najipodoa.

Tulikuwa na uhusiano naye kwa miezi sita na isitoshe alikuwa na bibi na watoto"

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be