#SemaNaRaey: Nina Miaka 21 Na Niko Kwa Ndoa Ya Tatu

anita raey
anita raey
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni, wahenga walinena.

Mwanadada mmoja shabiki sugu wa Redio Jambo alimuacha mtangazaji Anita Raey mwingi wa mshangao alipofichua kuwa kinyume na wenzake, ndoa kwake ni kama shule ya kujaribu ni kipi kinachoweza na ni kipi hakiwezi.

Hii ni baada ya mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 21, kusimulia kuwa amekuwa kwa ndoa tatu na kuwa hana nia ya kutulia hivi karibuni.

"Mimi niko kwa ndoa ya tatu na nina miaka ishirini na moja. Sasa unaeza fikiria ni ngapi nitawacha." Alijieleza huku akifichua kuwa kila ndoa amekuwa akidumu kwa mwaka mmoja pekee.

Kisa na maana, "Sasa unajua unaeza kutana na kijana mwingine huku nje msupuu kuliko mwenye yuko kwa nyumba, labda kuna vitu anakufanyia zenye bwanako hakufanyii.. sasa inabidi."  Aliongeza  huku akidai bado hana nia ya kutulia kwa ndoa moja.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be