Seneta wa kanti ya Bungoma Moses Wetangula awapongeza wabunge

Seneta wa kaunti ya Bungoma Moses Wetangula amewapongeza wabunge wa bunge la kitaifa kwa kutupilia mbali ripoti ya kamati maalum ya bunge kuhusu swala tata la sukari inchini.

Wetangula amesema kwamba ripoti hio iliyowakilishwa hapo jana bungeni ilikuwa haina uwazi ukweli na ililenga kuficha mabwenyenye ambao wanahusika na sukari hio ambayo si njema kwa matumizi.

Wetangula aidha ametaka serikali kuu kuajibika ipasavyo dhidi ya vita juu ya ufisadi na kupambana na waliohusika na sukari hio ambayo imeathri pakubwa uchumi wa maeneo ya ukuzaji wa sukari.

BRIAN O OJAMAA