Seneta Cleophas Malala atimuliwa chamani ANC

Osotsi na Malala
Osotsi na Malala
Chama cha  Amani National Congress kimefuta jina la Seneta wa Kakamega kutoka sajili.

Kamati ya nidhamu ya ANC ilifikia uamuzi huu Jumatano baada ya kufanya mkutano.

Taarifa kutoka kamati hiyo ya nidhamu inasema kwamba  Malala alimuunga mkono mgombea wa chama cha ODM katika uchaguzi mdogo wa Kibra.

Hii ni kinyume cha katiba na maagizo ya chama hicho.

"Baada ya kuchunguza kwa kina, NDC imeamua kuchuku hatua za kinidhamu kwa mwanachama huyo kutoka na sababu kwamba hatua zake zinaenda kinyume na sheria sio ya ANC lakini pia sheria za nchi," taarifa ilisoma.

Pia taarifa hiyo ilisoma kwamba, "NDC imeamua kumfurusha Cleophas Malala chamani ANC mara moja."

Katibu mkuu wa ANC Barrack Muluka alisema kwamba Malala ana siku 90 kupinga uamuzi huo wa kamati.

Hata hivyo hatua ya chama hicho kimepingwa na mbunge mteule Godfrey Osotsi.

Osotsi amesema kwamba uamuzi huo ni "utani mkubwa.'

Alisema kwamba  chama cha  ANC kilimteua Eliud Owalo kugombea uchaguzi wa Kibra bila kuwahusisha.