Seneta Olekina aperembwa laki 2 kwa facebook

LEDAMA 2
LEDAMA 2
Seneta wa Narok Ledama Olekina alipoteza shilingi laki mbili kwa mfanyibiashara laghai tarehe 3 mwezi Machi mwaka huu.

Seneta huyo kupitia facebook aliona mfanyibiashara huyo akiwa ameandika kwamba yeye hutoa huduma za ukulima wa ngombe wa maziwa pamoja na kujenga mabanda ya ng’ombe.

Kulingana na stakabadhi za mahakama,Ole Kina alipiga namabari za simu zilizokua zimewekwa katika ukurasa wa facebook wa kampuni ya Pensmart na kuzungumza na mtu kwa jina Njoroge, aliyempa namba mbadala kwa mawasiliano zaidi.

Njoroge alimuarifu Seneta Olekina kuwa ingekuwa vigumu kumpata afisini na kumtaka atumiye nambari hiyo mpya kumpata.

Baadaye Olekina alikutana na mfanyibiashara huyo katika eneo ambapo alidai kuwa ni ofisi yake kabla ya kuondoka kuelekea nyumbani kwa Olekina. Alimuonyesha mahali alikotaka kujenga mabanda hayo.

Waliafikiana kuwa Seneta huyo atalipa shilingi shilingi 320,000 na kazi kuanza mara moja na kisha akalipa sehemu ya kwanza ya shilingi laki mbili.

Baada wa wiki mbili, hakuna kazi iliyokuwa imefanyika na Njoroge alikuwa “ameingia gizani”. Majaribio ya kumpata alingonga mwamba na alipopatikana akatoa tena vijisababu.

Seneta Olekina kisha aliripoti kwa polisi, Njoroge alirejesha shilingi 50,000 na kudai kuwa hangeweza kufanya kazi ile na kwamba tayari alikuwa ametumia shilingi 150,000 kugaharamia mipango ya mradi huo.

Polisi walimkamata, jamaa huyo Peter Njoroge Nyondo afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Pesmart na kumfikisha mahakamani jana kwa kosa la kutumia ulaghai kupata pesa.

Alikanusha mashtaka na kuomba mahakama kumuachilia kwa dhamana. Hakimu Francis Andayi alikubali kumuachilia kwa dhamana ya shilingi 150,000 pesa taslim.

Kesi itatajwa Julai Mosi.