Seneta wa kaunti ya kakamega ateta juu ya gharama katika hospitali ya kaunti

Seneta wa kaunti ya kakamega Cleophas Malala, amevunja kimya chake kuhusu masaibu yanayowakumba wagonjwa katika kaunti ya kakamega kutokana na gharama ghali ya matibabu katika hospitali kuu ya kaunti ya Kakamega.

Hii ni baada ya wananchi kulalamika kuwa gharama ya matibabu katika hospitali hiyo imepanda kwa kiwango cha juu Zaidi.

Akihutubia wananchi mjini kakamega, Malala sasa anaitaka bunge ya kaunti hiyo kushirikiana na serikali ya kaunti na kuhakikisha kuwa gharama ya matibabu hospitalini humo inakuwa nafuu kwa wananchi wa kawaida.

Awali serikali ya kaunti hiyo kupitia kwa Gavana Wycliffe Oparanya ilisema kuwa gharama ya matibabu huamuliwa na serikali kuu kwa hospitali zote za rufaa nchini wala siyo serikali za kaunti.

Gavana huyo amesema kuwa wanampango wa kuhamasisha wananchi wa Kakamega umuhimu wa kujisajili na bima ya afya – (NHIF) ili waweze kukimu gharama ya matibabu kwenye hospitali za kiwango chochote nchini.