Seneta wa Lamu afurahia ujaza uzito wa bintiye Gavana Sonko, Saumu Mbuvi

Mwanawe gavana wa Nairobi, Saumu Mbuvi siku chache zilizopita alifichua kuwa mja mzito na mwenye mimba yake ni Seneta wa Lamu Anwar Loitiptip.

Saumu alisema kuwa hajajua jinsia ya mtoto ambaye amebeba, wawili hao wamekuwa katika mahusiano ya kimapenzi tangu mwaka wa,2019.

Alipoulizwa vile Seneta Loitiptip alipokea habari za uja uzito wake alijibu kwa ujasiri.

"Anwar ana furaha tele kuhusu mimba yangu, tulikuwa marafiki kabla tuanze kuchumbiana." Saumu Alisema.

Walipatana kwa mara ya kwanza mjini Mombasa ambapo Saumu alikuwa ameenda kujivinjari naye Seneta Anwar alikuwa kwa ziara ya kikazi.

" Namshukuru sana kwa maana yeye ndiye msaada wa mfumo wangu, huwa ananishauri ni sikubali jambo au mambo yasiyo ya maana kutawala maisha yangu." Saumu Aliongea.

Uhusiano wa awali kati ya Saumu na Ben Gatu ulivunjika kwa kile alikitaja kama uhusiano uliojaa vurugu.