Seneta wa Lamu Anwar Loitiptip Ashambuliwa vibaya na watu wasiojulikana

Seneta wa  Lamu  Anwar  Loitiptip  anauguza majeraha amabaya  katika hospitali ya  Aga khan baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana .

Kulingana na taarifa ya polisi  , Saumu Mbuvi ambaye ni bintiye Gavana wa Nairobi Mike Sonko alishuhudia tukio hilo . wawili hao walikuwa  pamoja .hizi hapa picha za taarifa aliondikisha  Saumu .

Saumu  amesema kabla ya shambulizi hilo walikuwa wakitazama fainali ya Uefa  katika   mkahawa wa  Memphis Lounge  katika mtaa wa kasarani .

Amesema wakati mchuano huo  ulipotamatika ndipo alipoviziwa na mwanaume mmoja aliyeanza kumshambulia   .

Ilikuwa ni wakati huo ambapo  seneta Anwar aiingilia kati  ili kumwokoa alipopiga kamsa .  wavamizi wengine kisha walijitokeza na kuanza kumshambulia Seneta huyo na kisha kumwangusha . saumu wanasema wanaume hao kisha walianza kumwomba msamaha seneta Anwar kabla ya kutoroka .

Wakielekea kwenye gari ,walikutana tena na genge na wanaume tisa waliokuwa  wamejihami kwa  rungu ambao walianza tena  kumshambulia seneta huyo . Saumu alipata majeraha ya mkoni alipojaribu kumkinga seneta Anwar.