Sensa: Fahamishwa kwa nini ngome za UhuRuto zitadhibiti uchaguzi wa 2022

Maeneo yanayodhibitiwa kisiasa na rais Uhuru Kenya pamoja na naibu wake William Ruto yana idadi kubwa sana ya watu huku takwimu zikionyesha ni karibu nusu ya milioni 47.6, ambayo ni idadi ya watu kulingana na sensa ya 2019.

Matokeo ya sensa ya mwaka huu inachora taswira rasmi kuhusu maeneo yaliyo na watu wengi na jinsi idadi hiyo itakavyoathiri uchaguzi wa 2022.

Kulingana na takwimu hizo za sensa, wanasiasa wanajua pa kusaka kura ifikapo uchaguzini.

Matokeo ya sensa ilidhirihisha kwamba ngome za Jubilee ambazo ni Mlima Kenya, Bonde la Ufa na Kaskazini Magharibi yana zaidi ya watu milioni 22.4.

Kulingana na idadi hii kubwa, maeneo hayo yatapata mgao mkubwa na pato la kitaifa kila mwaka.

Nazo ngome za kiongozi wa upinzani Raila Odinga ambazo ni Nyanza, Magharibi na Pwani zina idadi ya Wakenya milioni 16.4

Maeneo ya Kalonzo ambayo ni Ukambani yana milioni 3.5 ya Wakenya.

Ngome ya Naibu wa rais ambayo ni Bonde la Ufa iliorodheshwa kuwa na idadi ya milioni 11.7 ya watu.

Katika sensa ya 2009, Bonde la Ufa ilikuwa na zaidi ya watu milioni 9.2 hii ni kudhihirisha kwamba kwa mwongo moja, idadi imeongezeka kwa zaidi ya milioni 2.5.

Eneo la Mlima Kenya ambalo linajulikana sana kutokana na idadi kubwa ya wabunge, wameanza kupinga juhudi za kubadilisha mfumo wa utawala ambao unafutilia mbali mfumo ya rais kuchaguliwa katika bunge la kitaifa.