Serikali au Upinzani? Karua amkosoa Raila Kuhusu wajibu wa upinzani

Karua
Karua
Kiongozi wa chama cha Narc Kenya Martha Karua amemkosoa kiongozi wa ODM Rila Odinga  kuhusu matashi yake kwamba upinzani upo ndani ya serikali

Raila siku ya alhamisi alidai kwamba  chama cha ODM Kipo upinzani na pia serikalini . lakini karua ametumia mitandao ya kijamii kukosoa hilo akisema

" Ni mkanganyiko wa maksudi!  Katiba inaeleza kuwepo kwa  chama tawala kilicho serikalini na chama  cha upinzani  katika kiwango cha kitaifa na pia katika kaunti . kujifanfa kwamba upo ndani ya serikali nan je kama upinzani ni ukiukaji wa katiba !’ amesema Karua

Karua  amesema upinzani sasa ndio unaozungumza kwa niaba ya serikali .

"...  tunazungumza kuhusu ukosefu kabisa wa uangalizi  na wanachama cha chama cha wachache sasa wanazungumza kwa niaba ya serikali’ amesema Karua

Raila katika hotuba yake siku ya alhamisi alipuuza madai kwamba mwafaka wa handshake kati yake na rais Kenyatta umelegeza nguvu za upinzani .

Amesema sio jambo sawa kukitaraji chama cha ODM kuwa ndicho cha kuikosoa serikali .

" vyomvo vyetu vya habari havina ufahamu wa kutosha kuhusu wajibu wa chama cha ODM . kabla ya katiba mpya tulikuwa na mfumo wa mseto wa bunge na rais  ambapo upinzani uliangalia oparesheni za serikali  .katika mfumo wa sasa wa urais  ambapo kuna serikali ,bunge na idara ya mahakama  ,mambo ni tofauti’ Raila alisema

Raila amesema ni jukumu la bunge kuangalia shughuli za serikali kwa ushirikiano na chama cha walio wachache na sio jukumu la upinzani pekee