Serikali haitalegeza sheria kuhusu michezo ya kamari asema waziri Matiang’i

Serikali haina mpango wa kuyelgeza sheria kuhusu michezo ya kubashiri amesema waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i. Kuanzishwa kwa sheria hizo kali kulifanya kampuni nyingi za  michezo ya kubashiri kufungwa nchini na kulikuwa  matumaini kwamba huenda zikarejelea oparesheni baada ya kulegezwa  kwa baadhi ya sheria hizo .

Matiang’I aliyekuwa akizungumza katika taasisi ya KICD katika mkutano na viongozi kutoka Murang’a  amesema  amekuwa akipokea simu kutoka kwa viongozi wa kidini wanaohofia kwamba huenda michezo hiyo ya kubashiri ikirejea tena na kuwateka vijana baada ya sheria kulegezwa ili  kuruhusu kampuni hizo  ziendelee na oparesheni yazo nchini

“ Hatutabadilisha sheria hizo kwa sababu tunataka unadhifu enya .michezo ya kamari nusura iiharibu Kenya .wahalifu na watu  wanatakatisha fedha  walikuwa wakinawiri na wengine walikuwa wmetoka mashariki mwa Uropa.walikuwa wakifanya mambo ambao hawangeyafanya katika mataifa yao’ amesema Matiang’i

Waziri huyo  amesema  kwamba serikali inaheshimu uamuzi wa bunge kuhusu suala hilo  huku akiongeza  kwamba hakuna leseni iliyotolewa kwa kampuni ya michezo ya kubashiri mwaka huu wa kifedha  kwa sababu wanangoja idhini ya wizara ya afya  kwa ajili ya janga la corona .

Dr Matiang’I Pia amesema  serikali  hivi karibuni itaanzisha awamu ya pili ya msako dhidi ya  pombe haramu na  dawa za kulevya katika kaunti za Murang’a na Kiambu .