Serikali kufuata abiria,7,waliosafiri na mgonjwa mwenye virusi vya corona kutoka Nairobi hadi Bomet

Serikali ya kaunti ya Bomet wamo mbioni kuwatafuta abiria saba waliosafiri na mgonjwa aliyekuwa na virusi vya corona kutoka Nairobi hadi Bomet, hii ni kufuatia mgonjwa huyo kutolewa katika hospitali ya Nairobi kwa nia tatanishi.

Maafisa wa afya tayari wamemtenga mgonjwa huku wakizidi kuwatafuta abiria hao wengine.

Wizara ya afya imewataka abiria hao kujitokeza na kwenda kupimwa na kupokea matibabu kama watapatikana na virusi hivyo.

"We are making an appeal with the passengers who traveled to get in touch with our officer. Please reach out to our officer on this number 0726012387. You will be given instructions on what to do so that all of us are safe." Ujumbe wa gavana Hillary Barchok.

Maambukizi yanaonekana kusambaa na kuongezeka kila kuchao licha ya mipaka kufunguliwa na rais Kenyatta huku wananchi wengi wakifunga msafara na kuelekea mashambani.