Serikali kufungua uchumi wa taifa- Kibicho asema

Katibu katika wizara ya usalama wa ndani Karanja Kibicho amesema serikali inapania kufungua uchumi wa taifa huku masharti mengine mapya yakitazamiwa kuwekwa na serikali.

Akizungumza kwa mahojiano na stesheni ya Citizen, Kibicho amesema japo wazo hilo lipo mezani, masharti mengine huenda yakawekwa ili kuzuia maambukizi zaidi ya virusi hatari vya corona ambavyo vimekuwa  vikiongezeka kila uchao.

“We cannot lockdown forever, the government makes its money from taxes, currently people are not at work, personally I think we can re-open but under strict guidelines,”  Kibicho amesema.

Amesema japo baadhi ya masharti yatakuwa yakipunguzwa na serikali, vigezo vilivyowekwa vya kuvalia barakoa na kuzingatia umbali wa mita moja ni sharti utimizwe.

Amesema pia kampuni ambazo zinapania kurejelea hali yake ya kawaida ni vyema waangazie vigezo hivyo.

“Companies willing to re-open will need to ensure guidelines on facemasks and social distancing are adhered to because the new coronavirus is still here with us,” alisema Tuju.

Wakati uo huo amewataka wakenya kuendelea kuheshimu baadhi ya masharti yaliyowekwa na serikali kama njia ya kufanikisha vita dhidi ya virusi hivyo hatari.

Miongoni mwa masharti yanayotarajiwa kukamilika Jumamosi hii tarehe 6 ni kufungwa kwa miji mitano nchini ikiwemo Nairobi, Mombasa,Kwale, Kilifi na magatuzi mengine.