Serikali kutumia DNA kubaini miili ya watu Elgiyo Marakwet na West Pokot-Natembeya

unnamed (15)
unnamed (15)
NA NICKSON TOSI

Serikali sasa italazimika kupima chembe chembe za sampuli za watu yaani DNA kusaidia familia Elgiyo Marakwet na Pokot Magharibi kubaini miili ya wapendwa wao waliopoteza maisha kutokana na mafuriko yaliyoshuhudiwa eneo hilo.

Aghalabu watu 32 walipoteza maisha yao kutokana na mafuriko hayo ambayo pia yalibomoa nyumba zao na baadhi ya vituo vya polisi na shule  kaunti hizo mbili.

Kati ya watu hao 32,kumi na sita kati yao wangali hawajapatikana na kufikia sasa ni miili 4 tu iliyopatikana na huku iliyosalia ikiwa sehemu za miili ya watu ambao hawajulikana

“As per our records, 16 people are still missing, and we have only recovered body parts which cannot be identified except through DNA tests,”Mratibu wa  George Natembeya  amesema.

Natembeya amesema kuwa miili minne tu ndiyo iliyopatikana ikiwa na sehemu zote,na kuongeza kuwa asilimia kubwa ya watu walioaga dunia walitoka katika kaunti ya Elgiyo Marakwet,huku watu 150 wakilazimika kuhama makwao baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko.

Natembeya ameongeza kuwa sehemu za miili ya watu zilizopatikana zimehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Tot na Kapenguria.