Serikali kutumia milioni 350 kwa mafunzo, A-Z yaelezwa

ict
ict
Serikali imetangaza mipango ya kuwekeza zaidi ya shilingi milioni 350 katika mpango wa ukuzaji wa stadi kwa maafisa wa mawasiliano ya umma na habari.

Joe Mucheru ambaye ni waziri wa mawasiliano na teknolojia alisema kwamba fedha hizo zitatumika kuboresha na kuwasaidia maafisa hao wa serikali kutoa huduma bora.

 Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake katika mkutano huo wa PRSK uliofanyika mjini Mombasa, msemaji wa serikali Cyrus Oguna alisema kuwa serikali inaelewa mawasiliano ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Oguna aliongeza kuwa pesa hizo zilitengwa katika mwaka wa fedha uliopita ili kuhakikisha kuwa mawasiliano ya umma umeboreshwa.

Mucheru alisema kuwa serikali imeanza kutumia mfumo ambao unawajumuisha watu wote katika utoaji wa miradi ambayo inategemea sana maendeleo ya teknolojia.