Serikali ya Homa Bay yasubiri ripoti ya kubaini kilichosababisha kifo cha Mariam Awuor

unnamed (37)
unnamed (37)
Serikali ya Homa Bay sasa imesema itasubiri mwili wa mhudumu wa afya aliyefariki Mariam Awuor kufanyiwa upasuaji kubaini iwapo mhudumu huyo alifariki kutokana na corona.

Waziri wa afya kaunti hiyo Richard Muga amewataka Manesi pamoja na wahudumu wengine wa afya kuendelea kuchapa kasi pasi na uoga wowote .

Marian Awuor anasemerkana kufariki Jumapili asubuhi kutokana na matatizo mengine ya kiafya licha ya kupona kutokana na virusi vya corona.

Majuma mawili yaliyopita,Awuor alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi ICU baada ya kudaiwa kuwa alikuwa ameambukizwa virusi hivyo.

Mwendazake wa miaka 32 alikuwa anafanya kazi katika kituo cha afya cha Rachuonyo Kusini eneo la Oyugis na alikuwa mimba ya miezi mitatu .

Hii leo manesi wenzake wametaka serikali ya kuanti hiyo kuelezea ni nini kilichopelekea kifgo chake .

Chini ya muungano wao wa wahudumu wa afya KNUN,Katibu mkuu wa muungano huo George Bola amesema kuwa Awuor alijifungua vyema licha ya kufanyiwa upasuaji .

Amesema taarifa za kifo mwenzao ni za kushtusha kwani walikuwa wanatarajia kuwa ataruhusiwa kuondoka hospitalini hii leo.