Serikali ya Kenya yapiga marufuku watoto kutwaliwa na raia wa Kigeni

WAZAZI WAPANGAJI
WAZAZI WAPANGAJI
Baraza la mawaziri limepiga marufuku upangaji wa watoto na raia wa kigeni.

Kikao maalum cha baraza la mawaziri katika ikulu ya rais siku ya Alhamisi chini ya uwenyekiti wa rais Uhuru Kenyatta na kilichohudhuriwa na naibu rais William Ruto, kiliagiza wizara ya Leba na ulinzi wa kijamii kuunda sera maalum ili kudhibiti upangaji wa watoto na raia wa kigeni.

Mkutano huo pia uliagiza idara husika kulainisha oparesiheni za shirika la kushughulikia maslahi ya watoto pamoja na makao ya watoto. Agizo hilo linajiri wakati kuna utata unaozingira kesi iliohusisha mtoto mkenya, Baby Kiano aliyekuwa amepangwa na raia wawili wa kigeni.

Siku ya Jumatano Baby Kiano aliyekuwa ameondolewa kwa wazazi wake waliokuwa wamemchukuwa mwezi Aprili mwaka huu alirejeshewa wazazi hao. Duru katika shirika la watoto mtaani Lang’ata zilisema mtoto huyo alikabihdhiwa wawili hao baada ya mazungumzo marefu.

"Na thibitisha kuwa mtoto huyo amekabidhiwa wazazi waliomchukuwa saa tatu zilizopita katika hali isiojulikana,"