SGR kurejelea uchukuzi wa abiria Jumatatu wiki ijayo

macharia 1
macharia 1

Shughuli za uchukuzi wa abiria za gari la moshi la SGR kati ya miji ya Nairobi na Mombasa zitarejea Jumatatu wiki ijayo, waziri wa uchukuzi James Macharia amesema.

Hii ni baada ya kuwekwa kwa mikakati ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona katika uchukuzi wa abiria.

Soma pia;

Waziri siku ya Jumatano alisema kwamba safari ya kwanza kutoka Nairobi inatarajiwa mwendo wa saa mbili asubuhi na kuwasili mjini Mombasa saa sita mchana.

Gari hilo linatarajiwa kuondoka Mombasa kurejea Nairobi saa moja baadaye na kuwasili saa kumi na mbili jioni.

Macharia alisema wasafiri watakuwa na muda wa kutosha kufiki manyumbani mwao kabla ya muda wa kafyu saa tatu usiku.

Soma pia;

Waziri vile vile alisema kwamba shirika la Reli nchini Kenya Raiwalys litatoa mabehewa 10 ya kubeba abiria 600 ili kudumisha masharti ya umbali wa mita moja.

"Gari hilo litaruhusiwa kubeba asilimia 50 pekee ya kiwango chake cha abiria ," Macharia alisema.

Pia patakuwepo behewa moja la kuwatenga abiria wanaoonyesha dalili za virusi vya corona.

Serikali itatoa huduma za usafiri wa gari la moshi kuunganisha kituo cha SGR cha Nairobi katika eneo la Syokimau hadi katikati mwa jiji la Naiobi.

"Gari hili litakuwa likiondoka katikati mwa jiji la Nairobi saa saa kumi na mbili na dakika 35 asubuhi."

Soma pia;

Madaraka Express lilisitisha shughuli zake kutokana na mkurupuko wa virusi vya corona mwezi Machi.

Kurejeshwa kwa hudumu za gari moshi hili kunafuatia agizo la rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumatatu kulegeza masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya covid-19.

Wakenya hata hivyo wametakiwa kuajibikia matendo yao ili kuzuia usambaaji wa virusi hivi ambavyo kufikia sasa vimesababisha vifo kwa zaidi ya watu 160 humu nchini.