Shame on KDF: Tazama unyama ambao wanajeshi wawili walimfanyia kijana huyu huko Sotik

Victim
Victim
Polisi huko  Sotik katika kaunti ya Bomet wameanzisha uchunguzi kuhusu  tukio ambalo wanajeshi wawili wa Kenya army wanashtumia kwa kumshambulia mwanamme mmoja na kumjeruhi vibaya.

Kamanda  wa polisi katika eneo hilo  Francis Nganga  amesema tuko hilo lilifanyika katika kijiji cha Chebole siku ya jumatano .Kulingana  na Nganga wawili hao  Solomon Langat  na Leonard Kirui  wanaohudumu mombasa na Garissa mtawalia  walimvamia  Geoffrey Korir  mwenye umri wa miaka 25 katika kituo cha kibiashara cha Chebole alipokuwa akienda nyumbani .Nganga amesema wanajeshi hao wamekimbilia mafichoni baada ya unyama wao . Nganga amesema uchunguzi wa mwanzo umeonyesha kwamba wanajeshi hao walikuwa   wakilewa mchana  kutwa  katika eneo moja la burudani  katika sehemu hiyo .

Korir alikuwa akielekea nyumbani mwendo wa saa tano usiku baada ya kutazama mechi katika kituo hicho wakati wanajeshi hao walipomshambulia . Haijabainika kilichosababisha wawili hao kumshambulia na kumjeruhi vibaya raia  ambaye hakuwa amejihami wala kuwafahamu . Nganga amewataka wenyeji kuwa watulivu akiahidi kwamba wanajeshi hao wawili wataadhibiwa  kwa kukamatwa na kufikishwa kortini kwa  hatia ya kumshambulia na kumjeruhi raia .

Naibu mwenyekiti wa jamii ya wafanyibiashara katika eneo la chebole John Kirui amesema  wawili hao wana tabia ya kuwahangaisha raia wakati wanapokuwa nyumbani kwa likizo na kujigamba kwamba hakuna atakayewafanya lolote kwa sababu wao ni wanajeshi .

" Hatuna amani wakati wawili hao wanapokuja nyumbani .. ni watoto wetu  lakini wanatushambulia wakisema polisi hawawezi kuwakamata’ amesema .