Changamoto! Gavana Mutua awataka wanasayansi wa humu nchini kutafuta chanjo ya Coronavirus

NA NICKSON TOSI

Ni nini  ambacho wanasayansi na maprofesa wa humu nchini wanafanya kuhusiana na tishio la virusi vya Corona?, Wanasubiri wengine wafanye utafiti wa kupata dawa ya kutibu Corona?

Hayo ni maneno ya gavana wa Machakos Alfred Mutua ambaye amewakosoa wanasayansi na maprofesa wa humu nchini kwa kile amesema ni kulaza damu wakati wanasayansi kutoka mataifa mengine wanaendelea kufanya utafiti wa kupata tiba ya virusi vya corona.

Kufikia sasa, taifa la Kenya limesajili visa 59 vya watu ambao wameathirika na virusi hivyo baada ya kutangazwa kwa mara ya kwanza nchini mnamo Machi 13.

Kufikia sasa, watu zaidi ya alfu 40,000 kote ulimwenguni wameripotiwa kupoteza maisha yao na wengine laki nane.

Katika video kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii Gavana huyo aliwataka wanasayansi na wahadhiri wakuu kuamka usingizini na kutafuta kinga dhidi ya virusi vya Corona.

Mutua amekashifu hatua ya taifa hili kuendelea kuagiza dawa kutoka mataifa ya kigeni ilhali kuna uwezo wa Kenya kuanzisha vituo vya kutengeneza dawa humu nchini.

Usemi wake unajiri saa chache tu baada ya mhudumu wa afya kupatikana na virusi vya Corona katika kaunti ya Nairobi na kulazwa katika kituo kikuu cha kitaifa cha Mbagathi akiwa na mumewe.

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO