Shhh! Mwanamke ashtakiwa kwa kuwaita polisi ‘wafisadi’ Riruta

riruta
riruta
Mwanamke mmoja siku ya Jumanne ameshtakiwa  baada ya kuwaita polisi kuwa wafisadi katika kituo cha polisi cha Riruta.

Lonna Mwabishi  pia alishtakiwa kwa kumshambulia polisi mmoja mwanamke katika kituo hicho. Alishtakiwa kwa kusababisha usumbufu  na kuvuruga amani  baada ya kuwataja polisi kama ‘watu wafisadi ambao hutumia hongo kufanya ukahaba’.

Mwabishi anashtumiwa kwa kuyatekeleza makosa hayo yote  Julai tarehe tatu katika kituo cha Polisi cha Riruta, Nairobi.

Alifikishwa mbele ya  hakimu mkuu mkaazi wa kibera  Renee Kitagwa  ambapo alikana mashtaka dhidi yake.  Inadaiwa alimshambulia afisa wa polisi  Walloce Bundi.

Hata hivyo alikanusha mashtaka yote dhidi yake na kusema kwamba ni polisi hao ndio waliomshambulia. Amesema polisi walipendekeza mashtaka hayo dhidi yake ili kuficha ukatili wao. Aliachiliwa kwa  bondi ya shilingi 50,000 au dhamana ya shilingi 20,000 pesa taslimu.

Kesi hiyo itatajwa Julai  tarehe 21.