‘Shida ni kupata pesa!’ Joe Muchiri aomba msaada kumlipia Jowie dhamana ya millioni 2

Jow-Muchiri-with-Jowie-696x387
Jow-Muchiri-with-Jowie-696x387
Joe Muchiri ambaye ni rafiki karibu sana wa mshukiwa mkuu wa mauwaji ya mfanyabiashara Monica Kimani, Joseph Irungu'jowie'  ameomba wananchi na marafiki zake Jowie wamsaidie kupata millioni mbili  za kulipa dhamana alioachiliwa nayo na mahakama hii leo.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa twitter joe aliandika na kusema kuwa jowie yupo huru.

"Jowie Joe granted bail. FINALLY." Aliandika Muchiri.

Mahakama ya Milimani imemwachilia Jowie kwa dhamana ya millioni mbili.

Katika mtandao wake Joe aliandika na kuwataka wahisani wa karibu wa mshukiwa huyo kujitokeza na kusaidia kuchanga shilingi millioni mbili ambazo jowie aliachiliwa nazo kama dhamana.

"SHIDA SASA NI KUPATA HIO CASH BAIL YA JOWIE IMMEDIATELY. ITA BIDII WATU WALE WAKO ON HIS SIDE WAMECHANGAMKA. LETS’S SEE HOW THIS GOES." Alieleza.

Hakimu James Wakiaga alisema hakuna haja ya kumnyima mshukiwa dhamana na hivyo mahakama itakuwa ikienda kinyume na sheria.

Aliyeshtakiwa naye ambaye alikuwa kipenzi chake cha roho Jacque Maribe aliachiliwa kwa dhamana Octoba 2018.

Kupitia mtandao wake wa kijamii Muchiri aliongeza ujumbe ufuatao

"we are mobilizing for Jowie’s bail money granted by court which amounts to KSHS. 2,000,000/- we are kindly requesting for ur help in this time of need. If U can please send whatever U can to paybill 600100 account no. is 0100005024484 Stanbic Bank Please RT." Aliongeza Muchiri.