Shika Wezi wa Panties! Wanawake Murang'a waandamana kutokana na wezi wanaoiba panti

PF6IytFJ
PF6IytFJ
NA NICKSON TOSI

Kikundi cha wanawake katika kaunti ya Murang'a wameandaa maandamano kufuatia wizi uliokithiri eneo hilo wa surwali za ndani yaani panties.

Wanawake hao kutoka kijiji cha Mwirua wamesema wezi hao wamekuwa wakiiba kifuniko hicho cha asali kutokana na kile wamesema huwa wanaacha nje ili zikauke. Wameongeza kuwa hakuna kitu kingine kinachoibwa bali ni panties tu.

Wengine wamesema kuwa wamelazimika kubeba panties zao kwenye vipochi vyao kufuatia hatua ya wezi hao kuanza kuvunja milango na kuingia kwa nyumba.

"We are worried because these thieves are stealing women and girls' underwear while leaving men's on the line. We don't know what our children shall wear when schools re-open," wamedai wanawake hao.

Wengine wamedai kuwa chupi zinatumika sana katika mambo yanayohusika na ushirikina

"Maybe these thieves do not want our young girls to give birth when they come of age. I think they want to kill their 'Mandacu' (sexual health)," aliongeza mmoja wao.