Ripoti moja ya senate imeihusisha kemsa na kupotea kwa fedha katika mpango huo wa ununuzi wa mitambo ya hospitali kwa jina MES
Ufichuzi huo unalitia shirika hilo katika shinikizo Zaidi hasa wakati huu ambapo EACC inaendelea na uchunguzi mwingine kuhusu jinsi kemsa ilivyotumia mabilioni ya pesa za Covid 19 ili kununua vifaa vya kupambana na janga hilo .
Mameneja wa shirika hilo wakiongozwa na Afisa mkuu mtendaji Jonah Manjari aliyesimamishwa kazi walieleza jinsi walivyotoa kandarasi za mamilioni ya pesa kwa kampuni ambazo hazikustahili kupewa zabuni hizo na kukiuka sharia za uagizaji wa bidhaa .
Katika ripoti hiyo ya senate Kemsa inashtumiwa kwa kujipa jukumu la kuzichagua kampuni ambazo uwezo wake unatiliwa shaka kutoa mashine na vifaa vya matibabu vilivyohitajika chini ya mpango wa MES
Kemsa haikubaini iwapo vifaa na kemikali hizo zingeweza kununuliwa kutoka kwa kampuni nyingine kwa gharama ya chini .