Shirika La Kutetea Haki Za Binadamu Lataka Maafisa Wa GSU Kuchukuliwa Hatua

gsu-1
gsu-1
Shirika la kutetea haki za binadamu la Kenya Human Rights Watch magharibi mwa Kenya limetoa wito kwa waziri wa Usalama wa ndani Joseph Nkaiseri na mkuu wa polisi Joseph Boinet kuingilia kati na kuhakikisha kuwa maafisa wa polisi waliowadhulumu wakaazi wa Shibale Mumias wanatiwa nguvuni.

Mkurugenzi wa shirika hilo magharibi mwa Kenya, Peter Wanjala amesema wakaazi wa eneo hilo wanaishi katika hofu baada ya kudhulumiwa na maafisa wa polisi wanaotafuta bunduki zilizoibwa.

Akizungumza mjini Webuye na wanahabari baada ya kuzuru kijiji cha Shibale, Wanjala anataka wakaazi waliodhulumiwa kufidiwa akiwakashifu maafisa wa polisi kwa kutumia njia ya kimabhavu kuendeleza msako huo.

Hata hivyo, Wanjala amepuuzilia mbali hatua ya idara ya polisi kusema kuwa itamzawadi atakayetambua waliohusika katika wizi huo.