Shughuli ya kupima watu kuhusiana na corona yatatizika ghafla kaunti ya Kilifi

icfBsX_v
icfBsX_v
Uratibu wa kuanza kufanyia wakaazi wa kaunti ya Kilifi vipimo vya kubaini iwapo wameambukizwa virusi vya corona umetatizika baada ya kuanti hiyo kudai kuwa haina vifaa vya kutosha vya kufanikisha shughuli hiyo.

Kulingana na taarifa ni kuwa kaunti hiyo ya Kilifi ina wakaazi milioni 1.4 na vifaa ambavyo vilikuwa vimewasilishwa na serikali vina uwezo wa kubima wakaazi 300 pekee.

Kulinagana na wizara ya afya kaunti hiyo ya Kilifi ni miongoni mwa magatuzi ya humu nchini ambayo yanahitaji kuwafanyia wakaazi wake vipimo kutokana na idadi kubwa ya visa vya maambukizi yanayoripotiwa eneo hilo.

Katibu msimamizi katika wizara hiyo ya afya Dr Rashid Aman katika taarifa yake ya kila siku kwa taifa hiyo jana alisema kuwa serikali imeweka mikakati ya kuanza kuwapima wakenya katika maeneo tofauti ili kuwa na takwimu kamili za wale walioambukizwa.

Kufikia sasa, Kenya imesajili visa vya maambukizi 672 huku watu waliopona wakiwa 239.