Tume ya utumishi wa umma imepunguza shughuli zake ili kuzuia usambaaji wa virusi vya corona baada ya wafanyikazi wake 10 kupatikana na ugonjwa huo.
Kaimu mkurugenzi wa afya Patrick Amoth Jumanne alisema hatua nyingine kama vile kuhakikisha kwamba wafanyikazi hao hawakaribiani wanapokuwa kazini zimechukuliwa.
“Tutaweka mikakati katika afisi za serikali ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huu’ amesema Dr Amoth .
Afisa mkuu mtendaji wa PSC Simon Rotich amesema vipimo vilivyowalenga wafanyikazi wake vilionyesha kwamba kumi walikuwa na virusi hivyo.
Tume hiyo imesema oparesheni zake zitapunguzwa kwa siku 14 kuanzia Jumanne na kuja afisini sasa kutadhibitiwa miongoni mwa wafanyikazi wa tume hiyo.