Shughuli zimesitishwa katika mpaka wa Malaba baada ya madereva kufunga njia

EYmxREpXYAA84ok
EYmxREpXYAA84ok
Shughuli za usafiri katika mpaka wa Kenya na Uganda wa Malaba zimesitishwa baada ya madereva kutoka Kenya kushinikiza kuachiliwa kwa mmoja wao aliyezuiliwa na maafisa wa mpaka wa Uganda.

Jaribio hilo linajiri baada ya wiki mbili ambapo katibu mkuu wa muungano wa madereva wa masafa marefu Nicholas Mbugua kuwataka madereva hao kusitisha kabisa safari za Uganda.

Alhamisi madereva kupitia kwa mwenyekiti wa Muungano wao katika mpaka wa Malaba walishinikiza maafisa wa polisi kutoka Uganda kumwachilia mmoja wao ili akafanyiwe vipimo vya corona.

Wamesema kuwa mwenzao amekuwa akizuiliwa kwa muda wa saa 48 , hali inayotia maisha yake hatarini.

Pia wanapinga hatua ya maafisa wa Uganda kuchelewesha matokea yao ya vipimo katika mpaka huo. Wanasema kuwa baadhi yao ambao walifanyiwa vipimo Mei 16, hadi wa leo hawajapokea matokeo yao kamwe.

Kupitia Okeyo, sasa wanamtaka kiongozi wa taifa Uhuru Kenyatta kuzungumza na mwenzake wa Uganda ili kupata suluhisho kamili.

Wamesema hawasumbuliwi wanapokuwa wanaingia katika taifa jirani kama wanavyosumbuliwa na Uganda.

 “If a driver leaves Malaba going to Congo, he is not allowed to alight until he crosses in DR Congo,” Okeyo amesema.

Okeyo amesema kuwa maafisa wa Uganda wanaopima madereva wanaweka maisha yao hatarini kwani hawabadilishi glavu ambazo wanatumia.

 

“They don’t change their gloves and they can infect other people as they move about their business,” Okey amesema .