Shujaa Eliud Kipchoge atua Kenya kimya, mbwembwe na mapokezi hayapo

0_Eliud-Kipchoge-the-marathon-world-record-holder-from-Kenya-attempts-to-run-a-marathon-in-under-two
0_Eliud-Kipchoge-the-marathon-world-record-holder-from-Kenya-attempts-to-run-a-marathon-in-under-two
Nyota wa riadha Eliud Kipchoge amezuru nchini hii leo.

Kama desturi mtu an anapoenda nje na afanye kitendo cha ufanisi, mtu yule hukaribishwa kwa mbwembwe.

Makaribisho yaliyojaa furaha huwa ni sharti yaandaliwe ili kumpa heko kwa kazi nzuri.

Eliud Kipchoge alitwaa ushindi mkubwa Vienna na kwa hivyo alistahili makaribisho ya kishujaa.

Wengi walisubiri kuona mashabiki wakenya wakimpokea kwa tabasamu kubwa katika uwanja wa ndege.

Ulimwengu mzima ulimmulika nyota huyu huku rais wa Marekani Barack Obama akimhimiza zaidi.

Kupitia mtandao wa Twitter, Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama alitoa tamko la ushindi na kuunga mkono ushindi wa Eliud Kipchoge.

“Hapo jana (Jumamosi), Mkiambiaji Eliud Kipchoge amekuwa wa kwanza kuvunja rekodi ya masaa mawili. Hii leo (Jumapili)  Chichago, Brigid Kosgei ameweka rekodi mpya ya kidunia ya wanawake….Wawili hawa ni mfano mzuri wa uwezo wa binadamu kufaulu…” Obama.

Kama Eliud Kipchoge, Obama mwenyewe alitoa motisha kubwa zaidi kwa dunia baada ya kuchaguliwa kuiongoza Marekani.

Kitendo cha Eliud kutopokelewa kwa vifijo katika uwanja wa ndege kwa njia moja ama nyingine zinaonyesha nyufa zetu katika kuwatambua mashujaa wetu wanaoiuza nchi mbali.

Mtu na ambaye aliteka vichwa vya habari duniani nzima anapokelewa kikawaida tu nchi aliozaliwa ni jambo la kufedhehesha mno.

Au huenda Eliud Kipchoge hakutaka mbwembwe kama zile?

Je, mbona ulimwengu mzima umwangazie sana Eliud ilhali nyumbani hapokelewi kishujaa?