Muungano hu umesema hatua ya serikali kukosa kutoa pesa kwa shule hizo umezilazimu shule nyingi kuwatuma nyumbani wafanyikazi wake ambao wangesaidia katika kuhakikisha kwamba shule hizo hazigeuki kuwa mbuga kwani nyingi zina matatizo ya nyasi kumea na hata watu kuanza kuzitumia shule kama malisho ya mifugo .
Shule kadhaa zimelazimika kuuza mifugo yao kwa sababu ya kutoweza kuwalipa wafanyikazi wa kitunza na huko Nakuru shule nyingi zimetanagaza kwamba zinauza ngombe na nguruwe baadaya kukosa pesa za kuwalipa wafanyikazi wake .
Kampuni za ulinzi ambazo pia zimekuwa zikitoa huduma katika shule hizo zimeanza kujiondoa kwa kutolipwa hatua inayohatarisha mali ya thamani ya mamilioni ya pesa katika taasisi hizo .
Baadhi ya shule zimevamiwa na vifaa vya thamani kubwa kuibwa .
Mwenyekiti wa muungano huo katika kaunti ya Nakuru Fredrick Mbuthia amesema changamoto zinazokabili shule hizo zinazidi kuongezeka kila uchao .