Si akaunti yangu hiyo,asema Rayvanny

vanny
vanny

NA NICKSON TOSI

Msanii wa bongo Rayvanny ametupilia mbali madai kuwa akaunti yake ya Facebook ilitumiwa kumkejeli aliyekuwa baby mama wa Diamond Tanasha Donna.

Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Instagram, Rayvanny amewataka wanaotumia akaunti hiyo ya uongo kukoma kuendeleza uvumi huo na kuangazia shida zao ambazo zinawakumba.

Aliongeza kuwa hatumii vyovyote vile mtandao wa facebook na kuwarai wafwasi wake kutupilia mbali madai hayo.

“I DON'T USE THIS ACCOUNT!!!!!! THAT'S NOT ME 😡😡😡 ( RESPECT MY NAME) I DON'T USE FACEBOOK .......” alisema Rayvanny.

Akaunti inayotajwa kuwa ya uongo ilikuwa na ujumbe huu.

;“Asanteni kwa Watoto ..tumemalizana na East Africa Jee ..Mantaka Simba Asongee Nchi gani tena. Oooh!!! Poleni Bado Naskia Rwanda and Burundi ndo tumalizane na Mambo ya East Africa.”

Jumbe ziliibua hisia kinzani kutoka kwa baadhi ya wakenya ambao walitumia muda wao na kuanza kumkejeli msanii huyo ,wengine wakisema maneno yaliyotumika katika akaunti hiyo yalikuwa ya kukejeli.

Kando na Rayvanny kudai kuwa si ukurasa wake rasmi wa facebook,baadhi ya wafwasi wake walidai ni akaunti ambayo anatumia kutuma jumbe zake akiwa ametoa wimbo mpya.

Mashabiki walikuwa nahaya ya kusema kuhusiana na hatua hiyo

 “Yani ata iwe niwewe haiwezi stuka tabia zako hizo 🙈”

 “Aaiii and ur addressing it after 24hour datz was so trashy”

 “Kawadanganye wanyakyusa wenzio”

 “😭😭😭😭😭😭😭😭 RAY vany is not on Face Book 😭😭😭”

 “😂😂😂 boss wako atakumind mdogo Wang 😂😂”

 “🤣🤣bora mana hawachelewi kuongea ujinga”

 “Acha uongo vanny boy😂😂😂”

 “Sawa mzee Chui watu wanatembelea Nyota