'Si jambo la kawaida!' Vifo vya wazee vyatia hofu watu Nigeria

BUHARI-730x414
BUHARI-730x414
Mashirika na asasi zingine katika taifa la Nigeria Kaskazini haswa katika jimbo la Yobe yamesema watu 471 wamefariki kufikia sasa chini ya wiki tano, yakisema kuwa idadi hiyo ya watu ni ya kutiliwa shaka wakati huu ambao taifa hilo linakabiliana na corona.

Haijabainika wazi iwapo visa hivyo vinatokana na virusi hivyo.

Nigeria kufikia sasa limethibitisha visa vya maambukizi 5,000 huku watu 164 wakiwa wamefariki.

Mkuu wa Yobe Muhammad Lawan Gana ameliambia shirika la BBC kuwa baada ya utafiti kufanyika na bainika kuwa asilimia kubwa ya watu waliofariki ni wazee huku magonjwa kama kisukari yakiwa yanaendelea kuripotiwa.

Ameongeza kuwa baadhi ya watu hao wanaofariki walikuwa wameonyesha dalili za virusi vya corona.

Tumekuwepo na taarifa  kuwa asilimia kubwa ya vifo kutoka jimbo hilo la Yobe imekuwa ikifichwa swala ambalo limewapa wakaazi hofu.

Hatua ya kupima idadi ndogo ya watu katika taifa la Nigeria kubaini ni wangapi walioambukizwa virusi hivyo imetia hofu mashirika hayo yakisema huenda asilimia kubwa ya watu wanaishi na virusi hivyo