Siamini Barcelona walifanya kila wawezalo kumregesha Neymar - Messi

messi neymar
messi neymar
Lionel Messi amekiri kua haamini kwamba Barcelona walifanya kila wawezalo kumregesha Neymar Uhispania kutoka Paris Saint-Germain msimu huu wa joto.

Neymar alihusika katika mvutano mkubwa zaidi wa usajili msimu huu wa joto huku akitarajiwa kuwa angeregea Catalonia miaka miwili baada ya kuondoka kwa kitita kikubwa zaidi duniani.

Messi, ambaye alicheza vizuri na Neymar na Luis Suarez Barcelona, anasema angependa wajiunge tena.

VAR imefanya makosa manne kufikia sasa wakati wa msimu wa ligi ya Premier, mkuu wa marefa Mike Riley amekiri.

Mifano hiyo inajumuisha bao la kusawazisha la Fabian Schar kwa Newcastle dhidi ya Watford na bao la kiungo wa kati wa Leicester Youri Tielemans dhidi ya Callum Wilson wa Bournemouth, na ilijadiliwa jana katika mkutano wa wadau wa ligi ya Premier.

Makosa mengine mawili ni pamoja uamuzi wa refa wa kuwapa Manchester City penalti, Jefferson Lerma alipomkanyaga mguu David Silva katika kijisanduku cha Bournemouth, na uamuzi wa kuwanyima West Ham penalti Sebastien Haller alipoangushwa na Tom Trybull wa Norwich.

Tottenham huenda ikabadilishana kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen mwenye umri wa miaka 27, na mshambuliaji wa Juventus' raia wa Argentina Paulo Dybala wa miaka 25, wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari.

Kwingineko kiungo wa kati wa Manchester Paul Pogba alikuwa amekubali malipo ya mshahara wa pauni elfu 429 kwa wiki na Paris St-Germain kabla ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho lakini uhamisho huo uligonga mwamba baada ya Neymar kushindwa kuhamia Barcelona.

Mabingwa wa KPL Gor Mahia wanatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Algeria hii leo kwa mechi ya mkondo wa kwanza ya ligi ya mabingwa ya CAF dhidi ya USM Algiers.

Tukirejea humu nchini, safari ya Kogallo ilikua imekumbwa na tashwishi kutokana na ukosefu wa fedha lakini serikali ikaingilia dakika ya mwisho na kuwapa tikiti.

Klabu hio hata hivyo haijafahamu ni saa ngapi haswa watakapo ondoka nchini. Kogallo wanatarajiwa kuwasili Algeria kesho na watakua na chini ya masaa 24 kujitayarisha kwa mechi hiyo ya jumapili.

Timu ya raga ya wachezaji 15 kila upande huenda ikashiriki michuano ya four Nations cup itakayofanyika jijini Hong Kong mwezi Novemba. Kenya imeshawahi kushiriki kipute hicho huku shirikisho la raga duniani likiwalipia nauli za kusafiri na nchi waandalizi kuwapa malazi. Hata hivyo kulingana na KRU, timu hiyo itashiriki mashindano hayo iwapo tu watakua na pesa za kufadhili safari yao. Simbas kwa sasa wanajitayarisha kwa mechi ya Victoria cup dhidi ya Zimbabwe wikendi ijayo.

Majaribio ya riadha kuchagua timu itayoiwakilisha Kenya kwenye mashindano ya ubingwa wa dunia, yanaendelea leo katika uwanja wa Kasarani. Mbio zinazosubiriwa kwa hamu hii leo ni fainali ya kinadada ya mita elfu 5 huku Hellen Obiri akipigiwa upatu kushinda. Hata hivyo anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Agnes Tirop na Lillian Kasait aliyeshinda dhahabu katika All African Games. Fainali ya mbio za mita 1,500 kwa kinadada pia itaandaliwa leo huku Faith Chepngetich na Winny Chebet wakikimbia. Zitafuatiwa na za wanaume huku Timothy Cheruiyot na Elijah Manangoi wakitarajiwa kufufua uhasama. Mbio za mita elfu 3 kuruka viunzi kwa wanaume pia zitaandaliwa leo.

Timu ya voliboli ya kinadada ilifanya mazoezi yao ya kwanza huko Japan jana kablaya kuanza kwa kichuano ya kombe la dunia ya FIVB hapo kesho. Kinadada hao wanajitayarisha kwa mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Marekani kesho saa kumi na moja alfajiri. Hiki ni kipute cha pili cha kocha mkuu Paul Bitok baada ya kuwaongoza kwa ushindi katika All African Games. Bitok atachezesha kikosi alichokua nacho Morocco.