pjimage (14) (1)

Siasa haina mipaka ! Fahamu wanasiasa ambao ni mashemeji

NA NICKSON TOSI

Huenda baadhi ya wanasiasa nchini wanaegemea mirengo tofauti ya kisiasa lakini ikija upande wa maisha ya kibinafsi, wako na uhusiano mkubwa wa kijamii au kimaisha.

Hapa tumekuandalia orodha ya wanasiasa ambao wanaitana mashemeji labda kwa kuoa watoto wa wanasiasa wenzao au watoto wao kuoa kutoka familia ya wanasiasa.

1.Rais Kenyatta na Racheal Omamo

Mwanawe rais Kenyatta amemuoa mtoto wa Racheal Omamo Faith Achola.

Omamo ni waziri wa maswala ya Kigeni na awali alikuwa anashikilia wizara ya Ulinzi.

Jomo Kenyatta and his wife Achola

2. Mutahi Kagwe 

Waziri huyu wa afya amemuoa Ann Wanjiku Mutahi ambaye ni mtoto wa waziri wa zamani na marehemu John Michuki.

Wawili hao wamebarikiwa watoto wanne ambao ni Kagwe, Njoroge, Nyawira na  Kahumburu.

Former Nyeri senator Mutahi Kagwe and his wife Anne

3. Nelson Koech na Yvonne Kones

Nelson Koech ni mbunge wa Belgut kaunti ya Kericho na amemuoa mwanawe mbunge wa Bomet Beatrice Kones, msichana Yvonne Kones.

koech

 

 

 

 

 

4. Lavender Orengo

Kinara huyu wa wachache katika bunge la Seneti mwanawe Lavender Orengo alivuka na kuolewa labda si kutoka kwa familia inayofahamika sana kisisa lakini ameolewa na Hanington Muisyo Mutua kutoka kaunti ya Machakos.

5. Mr Adile Ramaphosa and  Bridget Birungu

Mwanawe rais wa Sasa wa Afrika Kusini ameoa msichana wa waziri mkuu wa zamani wa Uganda Amama Mbabazi.

Andile-and-Bridget-with-their-daughter

 

Mhariri: Davis Ojiambo

Photo Credits: Radio Jambo

Read More:

Comments

comments