Siasa za chacha: Mudavadi akutana na Peter Kenneth, Martha Karua na Sally Kosgei

885ab30b1722e3b4
885ab30b1722e3b4
Kiongozi wa chama cha Amani National Coalition Musalia Mudavadi alikutana na Martha Karua,Sally Kosgei na Peter Kenneth katika mkahawa mmoja jijini Nairobi Ijumaa, Mei 29 Ajenda ya mkutano wao haikubainika mara moja lakini wadadisi walisema lazima siasa zilishamiri.

Kila mwanasiasa anaonekana kujipanga kuhusu uchaguzi ujao wa 2022 ambapo Rais Uhuru atakuwa anaondoka Katika mkahawa mmoja jijini Nairobi, akina mama wawili waliketi upande mmoja wa meza na wanaume wawili upande wa pili. Kikao cha wanne hao kilionekana kuzungumzia masuala mazito huku wawili kati yao akipiga tama la kahawa.

Wanne hao walikutana katika kikao kinachodhaniwa kilikuwa cha kuchambua matukio yanayoendelea ya kisiasa. Mudavadi ni mmoja wa waliotangaza azma yao ya kuwania urais 2022 na kumrithi Rais Uhuru Kenyatta.

Imekuwa ni wiki ya matukio ya kisiasa huku vyama vya Jubilee na ODM vikionekana kujipanga kwa wimbi la kisiasa. Vinara Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta wanadadisiwa kupanga njama za kisiasa kuhusu uchaguzi wa 2022.

Huku Naibu Rais William Ruto, ambaye pia ametangaza azma ya kuwania urais 2022, akionekana kuandamwa na masaibu, Mudavadi naye amekuwa akikutana na wanasiasa mbali mbali.

Peter Kenneth na Martha Karua ni baadhi ya vigogo katika siasa za Mlima Kenya huku wote wakiwa wamewahi kugombea urais.

Sally Kosgei naye amekuwa ni mmoja wa viongozi wenye habari za kindani kuhusu masuala ya Ikulu baada ya kuwa mwandani wa aliyekuwa rais wa pili Daniel Moi.

Je wewe kama mwananchi unadhani walikuwa wanazungumzia nini haswa?