cleopas malala

Siasa za ubishi kati ya Cleopas Malala na mtangulizi Bonni Khalwale

Siasa za ubishi kati ya Seneta wa Kakamega Cleophas Malala na mtangulizi wake Bonni Khalwale zimewanasa wahudumu wa bodaboda, ambao sasa wanamtaka Khwalwale kuweka wazi ziliko zaidi ya shilingi milioni mbili unusu zilizochangiwa wanabodaboda mwezi Septemba mwaka jana na viongozi ambao walialikwa na Khalwale mjini Kakamega.

cleopas malala
Seneta wa kaunti ya Kakamega Cleopas Malala

Wahudumu hao wanadai Khwalwale hakuwahusisha kwenye harambee hiy,o licha ya kunuia kuwainua na alitumia kikundi ambacho hakina wanachama wa bodaboda.

“Bonni Khalwale leta pesa zenye Wetangula walisanya hapa za kununua pikipiki na uende uanunulie hao basi ambayo uliwaidi ya kupeleka watu Nairobi na kuwarudisha tena Kakamega,

“Hatuwezi kubali mtu aje kutukulia pesa zetu, tunataka tuone pesa zetu kwa maana sii ni wazee wa Kakamega,” Alisema mwendeshaji pikipiki.

Haya yamejiri siku moja baada ya Khalwale kumsuta malala kwa kuwandaa wanabiashara na kuwanunulia basi mzee baada ya kuchangiwa pesa na viongozi mwezi Disemba mwaka jana.

PATANISHO: Mama alimkosea mke wangu akitaka kujionesha yeye ndio kichwa

“Wanaume hawa wa pikipiki ndio wazee wetu na ni wao tunawetegemea,” Alieleza mama mmoja.

KATIKA KAUNTI HIYO: 

Mwanamume mwenye umri wa makamo amemuua mkewe na kisha kujitia kitanzi katika kijiji cha shinoyi kaunti ndogo ya navakholo kaunti ya Kakamega, kufuatia mzozo wa kimapenzi

Inadaiwa wawili hao walishiriki mapenzi nje ya ndoa yao na walizua ubishi ambao ulipelekea mauaji hayo.

ShowImage.ashx

“Mtu ana chukua bibi yake anapeleka kuenda kunywa pombe, kisha bwanake kumpeleka msichana, baada ya hapo mwanaume huyu aliweza kununua sumu,

“Nilisikia bibi yangu akiniita nikuje nione nilimuuliza ni nini kisha akaniambia mtoto anajinyonga,” Alisimulia Jirani.

Moses Kuria ataka wabunge kuangalia timu ya mawaziri ya Matiang’i

Baadhi ya wanajamii wanataka uchunguzi wa kimila na tambiko kutekelezwa kwani hiki ni kisa cha nne cha kujitoa uhai katika familia hiyo.

“Tuna mtoto wa kwanza alipatikana kwa kwamba, mwingine akakunywa sumu alafu mwingine wa miaka kumi alikufa kiholelaholela, kama deni semi tulipe kuliko hii kutendeka,” Jirani Alisimulia.

PIA SOMA:

Wauguzi katika kaunti ya Kakamega wataanza mgomo wao mwishoni mwa mwezi huu, iwapo serikali ya kaunti hiyo haitakuwa imetekeleza makubaliano ya malipo.

wauguzi
Wauguzi

“Tulikubaliana kabla ya jambo mbaya kutendeka majaliano na makubaliano itafanyika ambapo jambo hilo tumefanya,

“Kaunti ya Kakamega imekubali kutulipa pesa zetu mwishoni mwa mwezi wa pili, na wasipo fanya hivo naakikishia wauguzi kuwa tutagoma,” Alizungumza katibu wa wauguzi.

Katibu wa wauguzi kaunti ya kakamega Renson Lulunya, alisema wamepeana nafasi kwa makubaliano ya majadiliano na serikali ya kaunti kabla ya kuingia kwa mgomo.

Photo Credits: Google

Read More:

Comments

comments