SIAYA: Mbunge wa Alego aitaka serikali kuthibitisha sekta ya afya

Na Lameck Baraza kutoka jimbo la Siaya

Mbunge wa Alego Usonga anaitaka serikali kuu kurudisha wizara ya afya chini ya usimamizi wake ili kuzuiya visa vya migomo miongoni mwa wauguzi kila kuchao.

Muluan alielezea kuwa ni dhahiri serikali za kaunti hazina uwezo wa kuthibiti wizara ya afya na hivyo kuwasukumia wauguzi kuandaa mingomo wakidai haki zao.

Aliongezea kuwa ni jabo la kusikitisha kushuhudia wakenya wakikosa huduma za matibabu kutokana na maswala ambayo yanaweza kutatuliwa kwa njia ya majadiliano.

Aidha mwito wake unajiri baada ya wauguzi kususia kazi hapo jana wakidai nyongeza ya mishahara kwa asilimia 300 miongoni mwa mahitaji mengine.