Sidhani kama kunaweza kuwa na nafasi ya mke wa pili kama mimi ni wa kwanza-Aoko

aoko
aoko
Leo hii katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa naye Aoko Otieno, huku akizungmzia mambo kadha wa kadha, Aoko anafahamika sana kwenye mitandao ya kijamii ya twitter.

Aoko ni mtoto wa kwanza kati ya watoto tisa huku akisema kuwa anafuraha na mwenye bahati kuwa na mama wawili.

Akizungumzia jinsi huwa anawagandamiza wanawake kwenye mitandao ya kijamii alisema kuwa.

"Kwa muda mrefu sasa wanawake wamekuwa wakiwalaumu wanaume kwa shida ambazo wamepitia ama wanapitia pia wanaume wanashida ambazo wanakumbana nazo

Kama wanawake tunapaswa kujipigania kwa maana wakati umefika, mimi sijawahi kula nauli ya mwanamume lakini nikitumiwa naenda mahali uniambia niende

Kile najaribu kuambia wanawake ni kuwa tuna uwezo wa kuishi maisha yetu bila mwanamume katika maisha yetu." Alisema Aoko. 

Aoko alisema kuwa kuwa mwanamume ni kusimama na kufanya kazi yako ili mwanamume aitwe mwanamume,pia alisema kunatofauti ya kulala na mwanamume ambaye ni mume wa mtu, sponsor na mwanamume mzee.

Aoko ambaye ametoka katika familia ya mtala akizungumzia swala hilo alikuwa na haya ya kusema,

"Baba yangu ameoa bibi wawili, nafikiri aikuwa na sababu zake za kuoa mke wa pili,naweza kubali mume wangu aoe mke wa pili lakini kama mimi ni mke wa kwanza sidhani kama kuna weza kuwa na nafasi ya mke wa pili."

Kwa mengi zaidi tembelea mtandao wetu wa youtube.