Siendi ng'o!: Alexis Sanchez akiri hataondoka Man United

Mshambuliaji wa Manchester United na Chile Alexis Sanchez, 30, amekataa uhamisho wa kuelekea Roma, licha ya klabu hiyo ya Old Traford kukubali kulipa kitita kikubwa cha mshahara wake wa £560k kwa wiki.{Mirror)

Hatahivyo Sanchez huenda akaelekea katika ligi ya serie A baada ya Man United kumruhusu kufanya mazungumzo na Inter Milan, ambapo huenda akakubali kupunguza mshahara wake. (Mail)

Liverpool huenda ikafaidika na £18m iwapo mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo na raia wa Brazil Philippe Coutinho, 27, ataelekea Bayern Munich kwa mkopo. (Mail).

Everton imetoa ofa ya kumsaini winga wa Ufaransa Franck Ribery, 36, ambaye yupo huru baada ya kuondoka Bayern Munich baada ya kuhudumu kwa miaka 12 katika klabu hiyo ambayo ndio mabingwa wa ligi ya Bundesliga . (90Min)

Kwengineko, Kiungo wa kati wa Portugal Renato Sanches, 21, anataka kuondoka Bayern kwa kukosa muda wa kucheza katika klabu hiyo. (Sport1 - in German).

Mesut Ozil, 30, huenda akaondoka Arsenal na kujiunga na klabu ya DC United iwapo klabu hiyo ya ligi ya MLS inaweza kumshawishi kiungo huyo wa Ujerumani kuhamia Washington. (Star)

Beki wa kulia wa Ivory Coast Serge Aurier, 26, huenda akaondoka Tottenham na kuelekea AC Milan iwapo beki wa timu hiyo Andrea Conti, 25, ataondoka ligi ya Serie A kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho la Ulaya. (Calciomercato)

Na mchezaji wa Everton Yannick Bolasie, 30, yuko tayari kurudi katika uwanja wa Goodison Park, huku klabu za Uturuki Besiktas na Trabzonspor zikiwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa Congo . (Sun)

Mchezaji wa zamani wa Manchester City na Liverpool Mario Balotelli, 29, anakaribia kujiunga na klabu ya Serie A Brescia. (Sun via La Gazzetta)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 27, hakuorodheshwa katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya Rennes kutokana na jeraha na sio kwamba raia huyo wa Brazil anataka kurudi Barcelona. (AS - in Spanish)

Mshambuliaji wa Barcelona Kevin-Prince Boateng, 32, amefichua ni kwa nini Sir Alex Ferguson hakumsajili kujiunga na Manchester United mapema wakati wa kipindi chake cha mchezo. (Goal)

-bbc