Siendi popote Ruto awaambia wanaopenda ‘kulalamika’

Ruto
Ruto
Naibu wa rais  William Ruto amewashambulia viongozi ambao wana mazoea ya kumkosoa  kuhusu ukarimu wake na ziara zake katika sehemu mbali mbali za taifa .

" Sijui tatizo ni gani na baadhi ya watu . nawahurumia sana  .Nikiwaalika watu nyumbani kwani wana tatizo , nikienda kanisani wana tatizo ,nikitoa michango kuwasaidia watu ,wana tatizo,nikipena pikipiki wana tatizo’ alisema Ruto.

Aliongeza kusema ," iwapo una tatizo na shughuli zangu na vitendo vyangu basi utapata shida kwa muda mrefu kwa sababu siendi popote’

Alizungumza siku ya ijumaa  akiwa nyumbani kwake Sugoi wakati alipokutana na waakilishi wa kaunti  kutoka Trans Nzoia  kutoka vyama vya Jubilee , Ford Kenya na ANC

Ruto aliwashauri  wanaomkosoa kutumia maono ili kuwavutia wananchi badala ya kumkosoa .

" Nikipeana pikipiki wewe patia mtu mwingine gari … usiwe tu mtu wa kulalamika kila mara  …ukishindwa unalalamika ,ukiwa serikalini unalalamika …nimeunuliwa na Mungu ili pia mii niwainue wengine’

Mpinzani wa Ruto kiongozi wa ODM Raila Odinga na washirika wake wamekuwa wakimkosoa Naibu wa  Rais wa michango yake ya kila mara wakihoji alikotoa pesa hizo .

Wiki hii Raila aliomuonya Ruto dhidi ya kuliekeza taifa katika vita  baada ya washirika wa Ruo kumshambulia rais Kenyatta na familia yake .