Siezi jitoa uhai na nimwache mke wangu! Pastor Ng'ang'a asema

Mwanzilishi wa Neno Evangelism, mhubiri Ng'ang'a katika video amesema kuwa hajapanga kujiua kama inavyo daiwa na mashabiki wake.

Kulingana na mhubiri huyu, alisema kuwa ana sababu nyingi sana za kuishi na hivyo hawezi ata fikiria kuchukua maisha yake.

''Niliskia eti vyombo ya habari vimeandika eti Pastor Ng'ang'a anataka kugombea, kiti cha ubunge wa Kibra,really?

"Niliskia pia eti nilionekana nikiendesha  V8 eti nikiwa na huzuni kiasi cha kutaka kujitoa maisha."

"Tuwe 'serious' kwanza, nitajiua alafu nimwache bibi yangu mrembo hivi na nani,ataishi na nani? magari yangu nitayaacha na nani?'' Ng'ang'a alisema.

Zaidi ya hayo, aliuliza nani atarithi mali yake  iwapo atakufa.
Mhubiriri Ng'ang'a alisema pia, ikiwa watu hawajui, majirani wake ni wazungu, basi ni wazungu, na huwa wanasalimiana tu hakuna mambo ya kubisha mlango.

''INCASE YOU DID NOT KNOW MY NEIGHBORS ARE WAZUNGU’S WE JUST SAY ‘HI’ TO EACH OTHER HAKUNA MAMBO YA KUSHINDA TUKIBISHANIA MLANGO.''
 Licha ya hayo, alisema kuwa, watu wakimwita  fidhuli,''Arrogant,'' yeye anawaita Rubbish.Wanaosema kuwa nataka kujiua wajiue wenyewe kwanza.