Bi. Shollei alifanya kikao na wanahabari mjini Eldoret kwa muda wa dakika tano na hakukubali kujibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari . Amesema kamwe hatojibu maswali kuzihusu picha hizo au madai dhidi yake . ameongeza kwamba maajuzi ametishiwa kwamba jina lake litaharibiwa na anasema tukio hilo la kuzichaoisha picha hizo katika mitandao ya kijamii ni sehemu ya hila hizo dhidi yake .
Shollei amesema hakuna kampeini ya kumharibia jina itamzuia kuwahudumia wakaazi wa Uasin Gishu na taifa . Ameongeza kwamba licha ya picha hizo kusambazwa mtandaoni ameendelea kufanya kazi yake bila usumbufu wowote na hata alikuwa katika mahojiano ya runinga akizungumzia masuala yanayowaathiri wananchi wa eneo lake .
Shollei amesema changamoto zinazomkumba kwa sasa sio za kwanza na hazitadumu huku akishikilia kwamba ataendelea na majukumu yake ya kuwatunza watoto wake na kuwafanyia kazi wapiga kura .