Sijawahi beba mimba! Nadia Mukami akanusha uvumi kuhusu kutoa mimba ya Arrow

Nadia Mukami  hajamaliza kuzungumza kuhusu uhusiano wake wa zamani wa siri na msanii mwenzake  Arrow Bwoy.

Msanii huyo amekanusha madai kwamba  alitoa mimba  ya Arrow Bwoy. Wakati wa maswali na majibu katika ukurasa wake wa instagram, kuna shabiki  aliyetaka kujua iwapo ni ukweli kwamba Nadia alitoa mimba.

 “Ati ulitoa mimba ya Arrow Bwoy?” Shabiki mmoja aliuliza

Ingawaje swali hilo lilimpata ghafla, Mukami  alijibu kwa kusema kwamba hajawahi kupata mimba maishani mwake.

“Lmao!LoL! Sijawahi beba mimba. Children are a blessing and I can’t wait for that experience …..’ alisema

Mwingine alitaka kujua iwapo msanii huyo alikuwa single, Nadia alisema;

 “Single but I’m taking a time off to work on my self and let Love find me”.

Mwingine alimwambia kwamba Arrow Bwoy alipata mpenzi mwingine siku mbili baada yao kuachana.

“@nadia_mukami Kwani mliachana na Arrowboy?” asked Stivo Boy, to which Nadia responded saying: “@stivo_boy Alimove on na siku mbili.”

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO