Sijui mlienda meeting gani na dad ukasema twa twa - mwanawe Pastor Susan

pastor.susan.twa.twa
pastor.susan.twa.twa
Pastor Susan Munene wa kanisa la Hope Ministry Kasarani , amedokeza kuhusu jinsi walivyoipata taarifa ya video yake  twa twa ! ikisambaa mtandaoni.

Susan ambaye alikiri kwamba mapenzi huwa nguzo muhimu  kwenye ndoa, aliweka bayana kuwa ni kitendo hicho tu ambacho hudumisha na kuikuza ndoa.

Katika Show ya Bustani la Massawe Susana amefichua kuwa walikuwa wameenda kwenye shughuli zao za kila siku na waliporejea nyumbani na mumewe, watoto wao waliwapa habari hiyo.

"Kuna mahali tulikuwa tumeenda na Pastor wangu na tuliporejea nyumbani watoto wetu wakatuambia, Mom....dad, mnajua mnatrend.?

"Trending what ?" Aliuliza Susan.

"Sijui mlienda meeting gani mnaendanga na dad ukasema twa twa, sasa dunia imewaanika!" watoto waliuliza.

Aidha watoto wao waliendelea kusema, "Niliwaambia mufungue Youtube  channel kwa sababu mko na busara nyingi mkakataa na sasa mumeanikwa,"

"Watoto wenu ni wa umri mdogo na hamwoni wataathirika wakiwa shuleni wakiambiwa wazazi wao walitrend kuhusu suala ya mapenzi?" Massawe aliuliza.

"Tumewafunza kwamba mapenzi si ya watoto wachanga, vijana au matineja bali kwa wanandoa tu," alisema Susan.

Hata hivyo alikiri kwamba wanawe wangali wachanga na hutumia mitandao ya simu, lakini hao ndiyo huwadhibiti.

Licha ya kwamba ni watoto wao wa makasisi, Susan anasema  kwamba malezi ya wanawe huwa yamejikita kwenye Biblia.

"Tunawadhibiti kuhusu matumizi ya mitandao ya kijamii,"