traffic-police_0

Siku Za Mwizi ni 40, Jamaa Akamatwa Kwa Kumiliki Sare Za Polisi Migori

Polisi huko Rongo kwenye kaunti ya Migori wamemkamata mtu mmoja aliyekuwa ametoweka mara mbili kutoka mikononi mwa polisi alipokuwa amekamatwa kwa kumiliki sare za polisi pamoja na bunduki aina ya Ak 47 ambazo alikuwa akitumia kufanyia ujambazi mjini humo.

OCPD wa Rongo Jonathan Kisaka Muganda anasema ,mwanamume huyo ambaye alitambuliwa na umma na kisha waliowaarifu a polisi alikuwa ameenda mafichoni baada ya kutoroka mikononi mwa polisi aliyekuwa akimleta mahakamani mjini Migori mwishoni mwa mwaka uliopita na amekuwa akihepa mitego ya polisi lakini kwa sasa  anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kamagambo mjini Rongo.

Mshukiwa huyo anayetambulika kwa jina la utani Waiganjo atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kumiliki silaha ya bunduki na pia kutoweka kutoka mikononi mwa polisi mara mbili.

Photo Credits: file

Read More: Kisaka Muganda

Comments

comments