'Sikuwa nataka kumuoa,'Ringtone aeleza kwa nini alitaka kumpa Zari Hassan gari lake

Msanii wa nyimbo za injili Ringtone Apoko hatimaye amezungumza na kueleza kinagaubaga kwa nini alitaka kumpa Zari Hassan gari lake la Range Rover mwaka wa 2018.

Akiwa kwenye mahojino, Ringtone alisema kuwa hakuwa anataka kumuoa Zari bali alikuwa anataka kumpa moyo baada ya Zari kutengana na msanii wa bongo Diamond Platnumz.

Msanii huyo pia aliwashtumu na kuwalaumu wanahabari kwa kutafsiri vibaya habari hizo, alizidi na kueleza kisha kusema kuwa alimpenda Zari upendo wa kristo kwa maana yeye ni mkristu hamna cha kuongeza wala kupunguza.

"Zari sikuwa nataka kumuoa. Niliona Diamond amemuacha na anacomplain ati amekuwa heartbroken. Mimi kama mtumishi wa mungu nikaona nimuencourage. My first post nilisema Zari najua umeachana na Diamond ulishasema mwenyewe na kama unatafuta mwanaume hawezi kukuheartbreak ni yesu. Nikamwambia mimi kama Ringtone nakupenda kabisa venye yesu anakupenda."Alisema Ringtone.

Ringtone aliweka wazi kuwa alikuwa amempa gari lake la pesa nyingi yaani range rover kwa sababu aliona posti yake akiwa amesema kuwa anatamani gari la aina hiyo.

Na kwa maana alikuwa na gari nyingi za aina hiyo aliamua kumpa au kumzawidi gari hilo,

“Hio nilikuwa najaribu kumsaidia. Alikuwa amepost akisema anapenda range rover akapost ako na ya White, nikaona sababu nina nyingi na yeye ako na moja nikaona nimpe ya black." Alizungumza.

Alipoulizwa kwa nini hajaweza kuoa wala kuwa katika mahusiano na mwanamke yeyote alisema wanawake anaowapata wanataka umaarufu.

“Wasichana wengi wenye ninapata wanataka fame, na wanataka pesa. Because I decided washichana nimewaona lakini ule msichana natafuta sijamuona."Alieleza.

Zari na Diamond waliachana 2018, baada ya kuachana Zari alitua nchini kenya kwa miradi yake tofauti hapo ndipo Ringtone alipata fursa ya kumzawadi Zari.

Cha kushangaza mipango yake haikuenda vile alivyokuwa amepanga.