Simba! Je,Diamond Platinuz ‘Ataonja’ asali ya Afika Nzima ama ametosheka na Tanasha?Orodha Nzima ya Wapenzi wake wa zamani .

Staa  wa muziki wa Bongo Diamond Platinumz ametamba sana  kwa ajili ya muziki wake mzuri na wa kuvutia.

Nyota huyo hata hivyo pia amegonga vichwa vya habari kwa msururu wa vidosho ambao amehusiana nao na kisha kuwaacha hoi kila anapopata mpenzi mwingine. Diamond sio mgeni kwa sakata na amepata umaarufu sana wa kuweza kukana madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake kadhaa nchini Tanzania.

 

 Baada ya  kumuacha mpenziwe Tanasha Donna pekee yake katika hafla yake hapa Nairobi na kurejea Tanzania, wengi walishangaa ni kipi kilichomfanya  Simba kurejea TZ na kumuacha Tanasha pekee yake. Umeibuka sasa uvumi kwamba huenda Mondi alirejea Tanzania ili kuwa na wakati na  Hamisa Mobetto ambaye waliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi naye .

 Hawa hapa ni baadhi tu ya wanawake wanaojulikana kuwahi kuwa na uhusiano  na Diamond ingawa amekuwa akikana kuhusika katika mahusiano yoyote na baadhi yao.

Tanasha Dona

 Tanasha ndiye kipenzi kipya cha Diamond na  kimzaha penzi lao lilinawiri wakati  staa huyo alipoachana na  Zari. Wengi hawakuamini kwamba kulikuwa na uhalisia katika mipango yao ya kuishi pamoja kama wapenzi au mume na mke lakini wakathibitisha kwamba wapo ndano kwa muda mrefu ujao walipopata mtoto.

Hata hivyo  uhusiano wao pia upo  katika hali tete kwani hivi maajuzi, Diamond alimuacha Tanasha hapa jijini katika hafla yake na kurejea Bongo. Inadaiwa alipokuwa nyumbani, Simba alionekana na Hamisa Mobetto ! Haiwezi kutabirika kwa sasa iwapo Simba amefika kikomo  lakini  Diamond Platinumz hawezi kutabirika kweli.