SIMU KANDO! Wabunge wa Jubilee walizuiwa kuingia na simu kwenye mkutano wa Rais Uhuru KICC

8e74443ebdc9bd25
8e74443ebdc9bd25
Wabunge waliohudhuria mkutano wa Jubilee walitakiwa kuingia kwenye eneo la mkutano bila ya simu. Kulingana na maagizo tuliyoyaona, wajumbe walitakiwa kuwacha simu zao na wasaidizi.
"Hakuna simu kupita hapa," maagizo yalipewa wabunge kwenye mlango wa kuingia ukumbi wa KICC. 

Wabunge hao waliitwa kwenye mkutano huo ambapo Rais Uhuru Kenyatta alihudhuria. Ajenda ya mkutano huo haikuwa umebainiwa bali ulikuwa wa kumtimua Aden Duale kama kiongozi wa wengi bungeni.

Awali ilikuwa imearifiwa Rais atahutubia kikao hicho cha wabunge kupitia kanda ya video lakini hilo lilibadilika na Rais akakuwepo.

Mheshimiwa, tafadhali jua kiongozi wa chama atafika KICC saa tatu asubuhi kesho, Jumatatu Juni 22, 2020. Sisi wote tunafaa kuwa tumeketi kufikia 8:45am," wabunge walitumiwa ujumbe Jumapili, Juni 21, usiku. 

Naibu Rais William Ruto, ambaye pia ni naibu kiongozi wa chama alifika mapema kwenye ukumbi wa KICC. Mkutano huo ulisubiriwa kwa hamu na wadadisi ili kujua mabadiliko ambayo Rais atatangaza kwenye chama chake.

Aden Duale aling'atuliwa katika kiti cha kiongozi wa wengi bungeni na nafasi yake kuchukuliwa na Amos Kimunya.