Sina jibu mie! Kati ya hao wacheza santuri [DJ] nani mkali wao?

PhotoCollageEditor1587706366429
PhotoCollageEditor1587706366429
NA NICKSON TOSI

Kwa miaka mingi nchini kumekuwa na talanta kadhaa ambazo zimekuwa zikiibukia katika sanaa ya uchezaji santuri yaani DJ. Watu tofauti wamekuwa wakiingia na kupenye kwenye hii sanaa iliyojaa watu waliojenga jina loa tayari. Lakini kati ya hawa DJs ambao nimekuandalia hii leo, ni nani unayedhani kuwa ni bingwa kwa wote ama kazi yake inakubalika kuliko ya wengine.

1. Dj Joe Mfalme:

Mwaka 2009 alishindfa tuzo ya Inaugural Pilsner Mfalme  kwenye shindano lilokuwa limeandaliwa na kampuni moja ya vileo nchini.

Amekuwa akicheza miziki katika tamasha kuu za humu nchini kama; Airtel Trace Music Star, Koroga festival, Guinness made of black, Coke Studio Africa, Tusker Twende Rio promotion, Paris 7s after party na Luo festival.

2. Dj Bash:

Ni mcheza santuri katika redio moja ya humu nchini. Alizaliwa mwaka 1987 kutoka kwa familia ya watu walioenzi muziki na kutoka hapo akajipata katika tasnia hiyo ya kucheza miziki.

3. Dj Moh Spice:

Jina lake halisi ni Nicholas Mufo na ana miaka 32. Anapendelea sana kucheza miziki aina ya Reggae na alizaliwa kutoka familia ya watu waliokuwa wacheza santuri.

4. Dj Creme Dela Crème:

DJ Creme de la Crème, alinza taaluma yake ya kucheza miziki mnamo 2003 akiwa katika chuo kikuu cha Kabaraka . Kando na kuwa DJ, ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya kutengeza nguo za kisasa ya Epic Nation Clothing.

5.Vdj Jones:

Licha ya kuzaliwa katika vitongoji vya Usenge, alianzia taaluma yake kwa kucheza miziki  mitaani mwaka 2015 baada ya kumaliza shule ya Upili.

Mchanganyo wake wa miziki ulianza kunadi maskio ya watu wengi kwenye magari kama vile matatu, soko na hata nyumbani alikozaliwa.

6. Dj Lyta:

Ni miongoni mwa DJs ambao kwa miaka sasa wamekuwa wakifana zaidi katika taaluma hiyo. Licha ya kusomea maswala ya Teknolojia, Lyta alijikuta ameanza kucheza nyimbo kwa kujifunza taaluma hiyo kutoka kwa studio za rafikiye.

7. DJ Kym NickDee:

Ni kakaye mkubwa DJ Moh na kazi yake ya kucheza miziki inajulikana sana kutokana na uwezo wake wa kucheza miziki akishirikisha video mbalimbali.

DJ MELLOW

Ni miongoni mwa wanawake wanaofana sana katika taaluma hiyo iliyojaa wanaume tupu. Mellow alianza taaluma hiyo kwa kujifunza kutoka kwa wenzake waliomtangulia.

9. Dj Kris Darling:

Kris Darling ndiye aliyeanzisha kikundi cha  Dohty Family, ambacho huwaleta pamoja mamia ya DJs wanaocheza miziki ya Reggea. Alizaliwa katika mtaa wa mabanda wa Kibra Nairobi.

10. DJ Kalonje:

Amekuwa katika sanaa hiyo kwa miaka 10 sasa na ameshinda tuzo kama vile Chaguo la Teeniez.